Klabu ya soka ya Yanga wametetea ubingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa 2024/25. Yanga iliishinda mtani wake wa jadi Simba 2-0 katika mechi muhimu ya kuamua mshindi katika mechi iliyopigwa jijini Dar es salaam, Juni 25 2025. Huu ni ushindi wa nne mfululizo wa Yanga na wa 31.