THOMAS FULLER — KALKULETA YA BINADAMU KUTOKA AFRIKA!
Unamjua Thomas Fuller? Alizaliwa mwaka 1710 huko Benin, Afrika Magharibi. Akiwa na umri wa miaka 14 tu, aliuzwa kama mtumwa na kupelekwa Virginia, Marekani mnamo mwaka 1724.
Ingawa hakuwahi kwenda shule, Fuller alishangaza dunia kwa kipaji chake cha ajabu cha kufanya hesabu kichwani! Uwezo wake ulikuwa mkubwa kiasi cha kupewa jina la utani:
📌 "The Virginia Calculator" – Kalkuleta ya Virginia.
🧮 Siku moja, watu weupe waliomhoji walitaka kupima uwezo wake. Wakamuuliza:
❓ "Kuna sekunde ngapi katika mwaka mmoja na nusu?"
⏱️ Baada ya dakika mbili, alijibu: 47,304,000 — jibu sahihi kabisa!
Halafu wakaongeza swali gumu zaidi:
❓ "Mtu mwenye miaka 70, siku 17, na masaa 12, ameshaishi sekunde ngapi duniani?"
⏱️ Fuller alifikiria kwa dakika moja na nusu na kusema: 2,210,500,800 — tena, jibu sahihi kabisa!
😲 Watu waliokuwa wakimhoji walishangaa sana! Walisema hawajawahi kuona akili ya aina hiyo kwa mtu ambaye hajawahi hata kusoma darasani!
🕊️ Thomas Fuller alifariki mwaka 1790 akiwa na miaka 80.
🌍 Huyu ndiye Thomas Fuller – mfano wa wazi kuwa vipaji vya Waafrika havikuanza leo! Alikuwa kielelezo cha akili, uwezo, na ubinadamu wa watu weusi hata katikati ya mateso ya utumwa.
✊🏿 Tujivune na kusambaza historia kama hizi ambazo hazifundishwi darasani!
#ThomasFuller #HistoriaYaAfrika #BlackExcellence #Utumwa #KalkuletaYaBinadamu #Inspiration #TrueStory
