Nguli wa Barcelona, Andres Iniesta, anachunguzwa na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Umma nchini Peru kwa tuhuma za ulaghai wa takriban euro 518,000 (sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 1.4).
Kampuni zake, Never Say Never (NSN) Barcelona na NSN Sudamérica zinadaiwa kuandaa miradi ya burudani ambayo haikufanyika na kisha kushindwa kurejesha fedha za wawekezaji.
Miradi hiyo ilihusisha michezo ya kirafiki na tamasha la muziki wa K-pop ambayo hayakutekelezwa.
Inaelezwa Iniesta alipotoshwa na watu waliomzunguka, huku kampuni moja ikisemekana kuwa katika hatua ya kufilisiwa ili kulipa madeni.
Mwendesha mashtaka anaendelea kuchunguza iwapo fedha hizo zilihamishwa nje yabnchi. Iniesta hajatoa tamko rasmi kuhusu tuhuma hizo.
