Waziri Mkuu Mteule Dkt. Mwigulu Nchemba amekabidhiwa rasmi ofisi ya Waziri Mkuu

 Dodoma-

  1. Waziri Mkuu Mteule Dkt. Mwigulu Nchemba amekabidhiwa rasmi ofisi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika sherehe zilizofanyika katika ofisiza Waziri Mkuu zilizopo Mlimwa, Dodoma. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa serikali, pamoja na watumishi wa ofisi hiyo.


Katika tukio hilo, aliyekuwa Waziri Mkuu wa awamu iliyopita, Kassim Majaliwa, alikabidhi madaraka kwa Dr. Nchemba, ambaye sasa atachukua jukumu la kuongoza serikali katika kipindi kijacho. Viongozi wengine walioshiriki sherehe hiyo ni pamoja na aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu, Dr. Doto Biteko, katibu mkuu wa serikali, wakuu wa taasisi na idara mbalimbali, na watumishi wengine wa Ofisi ya Waziri Mkuu.


Dr. Mwigulu Nchemba, ambaye alikuwa ni Waziri wa Fedha na Mipango kabla ya uteuzi huu, alitumia fursa hiyo kuelezea ahadi yake ya kuendeleza juhudi za maendeleo na kuhakikisha utekelezaji wa mipango ya serikali inafanikiwa kwa manufaa ya wananchi. Aidha, alitoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua na kumwamini kushika wadhifa huu muhimu.



Kwa upande wake, Kassim Majaliwa alitoa pongezi kwa Dr. Nchemba na kumtakia kila la kheri katika utekelezaji wa majukumu yake. Alihakikishia ushirikiano wa kutosha kutoka kwa ofisi yake na wafanyakazi wa serikali ili kuhakikisha kwamba serikali inaendelea kutimiza majukumu yake ya kuwahudumia wananchi.


Sherehe hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali, watumishi wa serikali na wananchi, huku kukiwa na matukio ya kiutamaduni na burudani kutoka kwa vikundi vya sanaa vya kitaifa.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Popular Items