MOHAMED: KILA KIONGOZI AKIJIUZULU KISA NAFSI, HATUTAKUWA NA UONGOZI


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mohamed Kawaida amesema kama kila Kiongozi akijiuzulu kwa misingi ya maumivu ya nafsi hakutokuwa na Uongozi wa Taasisi bali wa hisia huku akimwambia Humphrey Polepole aliyejiuzulu Ubalozi wa Cuba kwamba hisia za Mtu binafsi haziwezi kuwa mizani ya uhalali wa uongozi wa Taifa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kawaida amesema “Kwako Polepole, hisia za Mtu binafsi haziwezi kuwa mizani ya uhalali wa uongozi wa Taifa, kukosa amani ya moyo ni hali ya nafsi binafsi, si hoja ya kimfumo, kama kila Kiongozi akijiuzulu kwa misingi ya maumivu ya nafsi, basi hatutakuwa na uongozi wa taasisi bali wa hisia, hulka sio nafsi”

Balozi wa Tanzania nchini Cuba na aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Humphrey Hesron Polepole alitangaza kujiuzulu Ubalozi jana July 13 2025 ambapo katika barua yake kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambayo ameichapisha katika kurasa za mitandao yake ya Kijamii jana Polepole amesema amefikia hatua hiyo baada ya tafakuri ya kina juu ya mwelekeo wa sasa wa uongozi Nchini.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post

Popular Items